Luke 20:3-8

3Akawajibu, “Nami nitawauliza swali. 4 aJe, ubatizo wa Yahya ulitoka mbinguni au kwa wanadamu?”

5Wakahojiana wao kwa wao wakisema, “Kama tukisema, ‘Ulitoka mbinguni,’ atatuuliza, ‘Mbona hamkumwamini?’ 6 bLakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu,’ watu wote watatupiga mawe, kwa sababu wanaamini kwamba Yahya alikuwa nabii.”

7Basi wakajibu, “Hatujui ulikotoka.”

8Isa akawaambia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.”

Mfano Wa Wapangaji Waovu

(Mathayo 21:33-46; Marko 12:1-12)

Copyright information for SwhKC